Amos 8:4-6

4 aLisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,
na kuwaonea maskini wa nchi,
5 bmkisema,

“Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita
ili tupate kuuza nafaka,
na Sabato itakwisha lini
ili tuweze kuuza ngano?”
Mkipunguza vipimo,
na kuongeza bei,
na kudanganya kwa mizani zisizo sawa,
6 cmkiwanunua maskini kwa fedha,
na wahitaji kwa jozi ya viatu,
na mkiuza hata takataka za ngano
pamoja na ngano.
Copyright information for SwhNEN